Malalamiko

1. Kwa Ujumla

Kama mmiliki wa leseni ya mbali ya michezo ya kubahatisha, 10bet lazima izingatie sheria zote za kamari, masharti ya leseni, kanuni za ufanyaji kazi na pamoja na miongozo mingine inayotumika kwa wenye leseni zilizotolewa na Mdhibiti.

2. Utaratibu wa kushughulikia malalamiko

Endapo mteja hajaridhika na matokeo au mrejesho wa ombi au swala ambao ameliwasilisha , au suala lolote linalohusu akaunti yake, wanaweza kuwasilisha malalamiko ya ndani.

Malalamiko yanaweza kuwasilishwa na wateja kwa njia ya maandishi kwa kupitia [email protected]

  • Endapo mteja anawasiliana na Huduma ya Wateja kupitia [email protected], Chatbot au fomu ya "Wasiliana Nasi", mtoa Huduma ya Wateja lazima amshauri mteja kupeleka malalamiko yake ya kina kwa maandishi kupitia:
  • Barua pepe: [email protected]
  • Mteja akiwasilisha malalamiko, taarifa ya kupokea kwa malalamiko hayo inapaswa kutolewa kwa mteja ndani ya masaa 72. Huduma kwa Wateja itapitia malalamiko na kuhakikisha kuwa ina taarifa zote muhimu ili kuichunguza, na ikiwa haina taarifa muhimu , Huduma kwa Wateja itamuomba mteja atoe taarifa zaidi inayohitajika.

Sehemu ya 12 ya Vigezo na Msharti ya 10bet imeeleza taarifa ambayo mteja anapaswa kuwasilisha wakati wa kuwasilisha malalamiko kwa mwendeshaji, kama:

  • Nambari ya simu ya mteja;
  • Jina la kwanza na la mwisho la Mteja, kama ilivyosajiliwa kwenye akaunti ya mteja;
  • Maelezo ya kina kuhusu malalamiko; na
  • Tarehe na muda maalum zinazohusiana na malalamiko.

Mara tu 10bet inapokuwa na taarifa zote muhimu, malalamiko yatapitiwa na timu ya Huduma kwa Wateja kwa tathmini na utatuzi.

Huduma kwaa Wateja inaweza kuhitaji msaada kutoka kwa Timu ya Utekelezaji. Kwa hali yoyote, mchakato wa kushughulikia malalamiko hautadumu zaidi ya siku kumi, isipokuwa kama malalamiko yamepelekea mazingira ya kipekee ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina na, katika hali kama hizo, Huduma kwa wateja itatuma barua pepe kwa mteja akielezea kwa nini 10bet haina jibu la mwisho, na kutaarifu muda unaotarajiwa kuwa na jibu moja.

Baada ya kukamilisha uchunguzi wowote muhimu, Huduma kwa Wateja itampelekea mteja uamuzi wa maandishi kuhusu azimio lililopendekezwa kutokana na malalamiko. Endapo malalamiko yamefanyiwa kazi na 10bet, na mteja hajaridhika na azimio hilo, mteja atajulishwa haki yake ya kupeleka suala lake kwa ajili Usuluhishi na msuluhishi mmoja aliyekubaliwa na pande zote kwa maandishi au kuwasiliana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha..

3. Taarifa kwa wateja

10bet lazima itoe taarifa kuhusu utaratibu wake wa kushughulikia malalamiko kwa wateja wake. Taarifa hizo lazima zijumuishe utaratibu, maelezo muhimu ya jinsi ya kuwasilisha malalamiko na maelezo ya mawasiliano yanayofaa pamoja na utambulisho wa vyombo vya usuluhishi kwa wateja. Wateja wana haki ya kuomba na kupokea nakala ya utaratibu kampuni wa kushughulikia malalamiko, kama ilivyoainishwa kwenye tovuti ya 10bet. Endapo ombi litatumwa, Huduma kwa wateja itawapatia taarifa hiyo kwenye mfumo wa PDF kwa njia ya simu au barua pepe.